Sunday, July 26, 2015

Aina za maneno

Nomino:Nouns
Viwakilishi:Pronouns
Vivumishi:Adjectives
Vitenzi:Verbs
Vielezi:Adverbs
Viunganishi:Conjunctions
Vihusishi:Prepositions
Vihisishi:Interjections

Saturday, April 26, 2014

Kontranimu

http://www.usingenglish.com/glossary/contranym.html

Wednesday, October 23, 2013

Friday, October 2, 2009

MUHTASARI WA NGELI ZA KISWAHILI

MUHTASARI WA NGELI ZA KISWAHILI

Meli K Wilson 2009

NGELI YA ....A-WA
Viashiria / Vionyeshi
huyu huyo yule
hawa hao wale
Mwanafunzi huyu ni mpole. Wanafunzi hawa ni wapole.
Chiriku huyo ataruka. Chiriku hao wataruka.
Nguruwe yule amenona. Nguruwe wale wamenona.

Viambishingeli (a-wa)
Mwanafunzi atasoma. Wanafunzi watasoma.

Kiunganifu a (wa-wa)
Mwanafunzi wa shule atie bidii. Wanafunzi wa shule watie bidii.

Matumizi ya –ote (wote-wote)
Mbuzi wote ameliwa. Mbuzi wote wameliwa.

Matumizi ya o-o-te (yeyote-wowote)
Mkulima yeyote asiwe mvivu. Wakulima wowote wasiwe wavivu.

Matumizi ya -ngi (- wengi) .
Wazee wengi wamefika mkutanoni.

Matumizi ya -ngine (mwingine-wengine)
Msichana mwingine aje hapa. Wasichana wengine waje hapa.

Matumizi ya -enye (mwenye – wenye)
Mvuvi mwenye uvivu hafanikiwi. Wavuvi wenye uvivu hawafanikiwi.

Matumizi ya -enyewe (mwenyewe – wenyewe)
Chura ameruka mwenyewe. Vyura wameruka wenyewe.

Matumizi ya -ndi- (ndiye- ndio)
Simba ndiye aliyemwua nyati Simba ndio waliowaua nyati.

Matumizi ya si- (siye- sio)
Mtu mwoga siye atumwaye. Watu waoga sio watumwao.

Matumizi ya na- (naye- nao)
Nyuki naye ametua uani. Nyuki nao wametua mauani.

Kirejeshi amba- (ambaye- ambao)
Ndege ambaye anaimba yu mtini. Ndege ambao wanaimba wa mitini.

Kirejeshi o awali (ye- o)
Ndege anayeimba yu mtini. Ndege wanaoimba wa mitini.

Kirejeshi o tamati (ye- o)
Ndege aimbaye yu mtini. Ndege waimbao wa mitini.

UKANUSHAJI KATIKA NYAKATI MBALIMBALI
Wakati uliopita (li)
Mimi nilikisoma kitabu hiki. Mimi sikukisoma kitabu hiki.
Sisi tulivisoma vitabu hivi. Sisi hatukuvisoma vitabu hivi.

Wewe ulienda mjini. Wewe hukuenda mjini.
Nyinyi mlienda mijini. Nyinyi hamkuenda mijini.

Yeye aliipenda anasa. Yeye hakuipenda anasa.
Wao walizipenda anasa. Wao hawakuzipenda anasa.
Wakati timilifu (me)
Mimi nimekisoma kitabu hiki. Mimi sijakisoma kitabu hiki
Sisi tumevisoma vitabu hivi. Sisi hatujavisoma vitabu hivi.

Wewe umeenda mjini. Wewe hujaenda mjini.
Nyinyi mmeenda mijini. Nyinyi hamjaenda mijini.

Yeye ameipenda anasa. Yeye hajaipenda anasa.
Wao wamezipenda anasa. Wao hawajazipenda anasa.
Wakati uliopo (na)
Mimi ninakisoma kitabu hiki. Mimi sikisomi kitabu hiki.
Sisi tunavisoma vitabu hivi. Sisi hatuvisomi vitabu hivi.

Wewe unaenda mjini. Wewe huendi mjini.
Nyinyi mnaenda mijini. Nyinyi hamwendi mijini.

Yeye anaipenda anasa. Yeye haipendi anasa.
Wao wanazipenda anasa. Wao hawazipendi anasa.
Wakati ujao (ta)
Mimi ni nitakisoma kitabu hiki. Mimi sitakisoma kitabu hiki.
Sisi tu tutavisoma vitabu hivi. Sisi hatutavisoma vitabu hivi.

Wewe utaenda mjini. Wewe hutaenda mjini.
Nyinyi mtaenda mijini. Nyinyi hamtaenda mijini.

Yeye ataipenda anasa. Yeye hataipenda anasa.
Wao watazipenda anasa. Wao hawatazipenda anasa.

NGELI YA ....KI-VI
Viashiria / Vionyeshi
hiki hicho kile
hivi hivyo vile
Kioo hiki kimepasuka. Vioo hivi vimepasuka.
Chungu hicho ni cha zamani. Vyungu hivyo ni vya zamani.
Kitoto kile kinapenda kulialia. Vitoto vile vinapenda kulialia.

Viambishingeli (ki-vi)
Chakula kikipikwa nitakila. Vyakula vikipikwa tutavila.
Kiunganifu a (cha-vya)
Kikombe cha chai kipo. Vikombe vya chai ni vipo.
Matumizi ya ote (chote-vyote)
Kijiji chote kimeshangazwa. Vijiji vyote vimeshangazwa.
Matumizi ya -o-o-te (chochote-vyovyote)
Kijizi chochote kitashikwa. Vijizi vyovyote vitashikwa.
Matumizi ya -ngi (kingi- vingi)
Kileo kingi kisinywewe. Vileo vingi visinywewe.
Matumizi ya -ngine (kingine-vingine)
Kiatu kingine ki wapi? Viatu vingine vi wapi?
Matumizi ya -enye (chenye – vyenye)
Hiki ni kitoweo chenye pilipili. Hivi ni vitoweo vyenye pilipili.
Matumizi ya -enyewe (chenyewe-vyenyewe)
Kitabu chenyewe kina hadithi.. Vitabu vyenyewe vina hadithi.
Matumizi ya -ndi- (ndicho-ndivyo)
Kilima ndicho kilichonichosha. Vilima ndivyo vilivyotuchosha.
Matumizi ya si- (sicho-sivyo)
Kikombe hiki sicho changu. Vikombe hivi sivyo vyetu.
Matumizi ya na- (nacho- navyo)
Chungu nacho kina manufaa. Vyungu navyo vina manufaa.
Kirejeshi amba- (ambacho- ambavyo)
Kioo ambacho kinatumiwa ni kipya. Vioo ambavyo vinatumiwa ni vipya.
Kirejeshi o awali (cho-vyo)
Kioo kinachotumiwa ni kipya. Vioo vinavyotumiwa ni vipya.
Kirejeshi o tamati (cho-vyo)
Kioo kitumiwacho ni kipya. Vioo vitumiwavyo ni vipya.

UKANUSHAJI KATIKA NYAKATI MBALIMBALI
Wakati uliopita (li) (hakiku-haviku)
Kioo kilinunuliwa. Kioo hakikununuliwa.
Vioo vilinunuliwa. Vioo havikununuliwa.
Wakati timilifu (me) (hakija-havija)
Kioo kimenunuliwa. Kioo hakijanunuliwa.
Vioo vimenunuliwa. Vioo havijanunuliwa.
Wakati uliopo (na) (haki-havi)
Kioo kinanunuliwa. Kioo hakinunuliwi.
Vioo vinanunuliwa. Vioo havinunuliwi.
Wakati ujao (ta) (hakita-havita
Kioo kitanunuliwa. Kioo hakitanunuliwa.
Vioo vitanunuliwa. Vioo havitanunuliwa.

NGELI YA ....U-I
Viashiria / Vionyeshi
huu huo ule
hii hiyo ile

Mti huu umesitawi vyema. Miti hii imesitawi vyema.
Mlima huo una theluji. Milima hiyo ina theluji.
Mkahawa ule ulinipendeza. Mikahawa ile ilitupendeza.

Viambishingeli (u-i)
Mwembe ule unao embe tamu. Miembe ile inayo maembe matamu.
Kiunganifu a (wa-ya)
Mkate wa leo ni mtamu. Mikate ya leo ni mitamu.
Matumizi ya ote (wote-yote)
Mkono wote uwe safi. Mikono yote iwe safi.
Matumizi ya - o-o-te (wowote-yoyote)
Mundu wowote sio mkali. Miundu yoyote siyo mikali.
Matumizi ya -ngi (mwingi- mingi)
Muwa mwingi hautafuniki. Miwa mingi haitafuniki.
Matumizi ya -ngine (mwingine-mingine)
Mto mwingine umefurika. Mito mingine imefurika.
Matumizi ya -enye (wenye – yenye)
Mkebe wenye maji umeanguka. Mikebe yenye maji imeanguka.
Matumizi ya -enyewe (wenyewe-yenyewe)
Mgongo wenyewe umeumia Migongo yenyewe imeumia.
Matumizi ya -ndi- (ndio-ndiyo)
Mhindi ndio utakaositawi haraka. Mihindi ndiyo itakayositawi haraka.
Matumizi ya si- (sio-siyo)
Mzigo wako sio mzito. Mizigo yenu siyo mizito.
Matumizi ya na- (nao- nayo)
Mshahara huo nao haumtoshi. Mishahara hiyo nayo haiwatoshi.
Kirejeshi amba- (ambao- ambayo)
Mti ambao unakatwa ni wake. Miti ambayo inakatwa ni yao.
Kirejeshi o awali (o-yo)
Mti unaokatwa ni wake. Miti inayokatwa ni yao.
Kirejeshi o tamati (cho-vyo)
Mti ukatwao ni wake. Miti ikatwayo ni yao.

UKANUSHAJI KATIKA NYAKATI MBALIMBALI
Wakati uliopita (li) (hauku-haiku)
Mlango ulifungwa. Mlango haukufungwa.
Milango ilifungwa. Milango haikufungwa.
Wakati timilifu (me) (hauja-haija)
Mlango umefungwa. Mlango haujafungwa.
Milango imefungwa. Milango haijafungwa.
Wakati uliopo (na) (hau-hai)
Mlango unafungwa. Mlango haufungwi.
Milango inafungwa. Milango haifungwi.
Wakati ujao (ta) (hauta-haita)
Mlango utafungwa. Mlango hautafungwa.
Milango itafungwa. Milango haitafungwa.

NGELI YA ....I-ZI
Viashiria / Vionyeshi
hii hiyo ile
hizi hizo zile

Kalamu hii ni nzuri. Kalamu hizi ni nzuri.
Ndoo hiyo inavuja. Ndoo hizo zinavuja.
Habari ile ni muhimu. Habari zile ni muhimu.

Viambishingeli (i-zi)
Shule itafunguliwa. Shule zitafunguliwa.
Kiunganifu a (ya-za)
Siku ya sherehe imewadia. Siku za sherehe zimewadia.
Matumizi ya ote (yote-zote)
Karatasi yote imechafuka. Karatasi zote zimechafuka.
Matumizi ya - o-o-te (yoyote-zozote)
Nyumba yoyote ni makao. Nyumba zozote ni makao.
Matumizi ya -ngi (nyingi)
Nchi nyingi haziendelei kiuchumi.
Matumizi ya -ngine (nyingine-nyingine)
Redio nyingine ifunguliwe. Redio nyingine zifunguliwe.
Matumizi ya -enye (yenye – zenye)
Nguo yenye uchafu itafuliwa. Nguo zenye uchafu zitafuliwa.
Matumizi ya -enyewe (yenyewe-zenyewe)
Barua yenyewe haijatumwa. Barua zenyewe hazijatumwa.
Matumizi ya -ndi- (ndiyo-ndizo)
Sabuni ndiyo iliyopotea. Sabuni ndizo zilizopotea.
Matumizi ya si- (siyo-sizo)
Habari ile siyo iliyotarajiwa. Habari zile sizo zilizotarajiwa.
Matumizi ya na- (nayo- nazo)
Hata meza nayo ipakwe rangi. Hata meza nazo zipakwe rangi.
Kirejeshi amba- (ambayo- ambazo)
Njia ambayo inapitiwa ni ndefu. Njia ambazo zinapitiwa ni ndefu.
Kirejeshi o awali (yo-zo)
Njia inayopitiwa ni ndefu. Njia zinazopitiwa ni ndefu.
Kirejeshi o tamati (yo-zo)
Njia ipitiwayo ni ndefu. Njia zipitiwazo ni ndefu.

UKANUSHAJI KATIKA NYAKATI MBALIMBALI
Wakati uliopita (li) (haiku-haziku)
Ngoma ilipigwa. Ngoma haikupigwa.
Ngoma zilipigwa. Ngoma hazikupigwa.
Wakati timilifu (me) (haija-hazija)
Ngoma imepigwa. Ngoma haijapigwa.
Ngoma zimepigwa. Ngoma hazijapigwa.
Wakati uliopo (na) (hai-hazi)
Ngoma inapigwa. Ngoma haipigwi.
Ngoma zinapigwa. Ngoma hazipigwi
Wakati ujao (ta) (haita-hazita)
Ngoma itapigwa. Ngoma haitapigwa.
Ngoma zitapigwa. Ngoma hazitapigwa.

NGELI YA ....LI-YA
Viashiria / Vionyeshi
hili hilo lile
haya hayo yale

Shati hili ni chafu. Mashati haya ni machafu.
Jino hilo litang’olewa. Meno hayo yatang’olewa.
Jibwa lile ni kali. Majibwa yale ni makali.

Viambishingeli (li-ya)
Jikombe la jitu limejaa maji. Majikombe ya majitu yamejaa maji.
Kiunganifu a (la-ya)
Jambo la maana limenenwa. Mambo ya maana yamenenwa.
Matumizi ya ote (lote-yote)
Jiti lote litatupwa. Majiti yote yatatupwa.
Matumizi ya - o-o-te (lolote-yoyote)
Shauri lolote lisipuuzwe. Mashauri yoyote yasipuuzwe.
Matumizi ya -ngi (mengi)
Machungwa mengi yameiva.
Matumizi ya -ngine (jingine-mengine)
Embe jingine litaliwa. Maembe mengine yataliwa.
Matumizi ya -enye (lenye-yenye)
Rinda lenye uchafu lifuliwe. Marinda yenye uchafu yafuliwe.
Matumizi ya -enyewe (lenyewe-yenyewe)
Yai limeanguka lenyewe. Mayai yameanguka yenyewe.
Matumizi ya -ndi- (ndilo-ndiyo)
Shimo ndilo lililochimbwa. Mashimo ndiyo yaliyochimbwa.
Matumizi ya si- (silo-siyo)
Ua hili silo zuri kwani halinukii. Maua haya siyo mazuri kwani hayanukii.
Matumizi ya na- (nalo- nayo)
Pera nalo lina mbegu nyingi. Mapera nayo yana mbegu nyingi.
Kirejeshi amba- (ambalo- ambayo)
Jino ambalo linauma ling’olewe. Meno ambayo yanauma yang’olewe.
Kirejeshi o awali (yo-zo)
Jino linalouma ling’olewe . Meno yanayouma yang’olewe.
Kirejeshi o tamati (lo-yo)
Jino liumalo ling’olewe. Meno yaumayo yang’olewe.

UKANUSHAJI KATIKA NYAKATI MBALIMBALI

Wakati uliopita (li) (haliku-hayaku)
Wingu lilitanda. Wingu halikutanda.
Mawingu yalitanda. Mawingu hayakutanda.
Wakati timilifu (me) (halija-hayaja)
Wingu limetanda. Wingu halijatanda.
Mawingu yametanda. Mawingu hayajatanda.
Wakati uliopo (na) (hali-haya)
Wingu linatanda. Wingu halitandi.
Mawingu yanatanda. Mawingu hayatandi.
Wakati ujao (ta) (halita-hayata)
Wingu litatanda. Wingu halitatanda.
Mawingu yatatanda. Mawingu hayatatanda.

NGELI YA ....U-YA
Viashiria / Vionyeshi

huu huo ule
haya hayo yale
Uamuzi huu ni mwema. Maamuzi haya ni mema.
Upishi huo uliudhi. Mapishi hayo yaliudhi.
Ulili ule umeletwa. Malili yale yameletwa.

Viambishingeli (u-ya)
Ugonjwa umezidi. Magonjwa yamezidi.
Kiunganifu a (wa-ya)
Upishi wa mama ni mzuri. Mapishi ya akina mama ni mazuri.
Matumizi ya ote (wote-yote)
Uasi wote umekomeshwa. Maasi yote yamekomeshwa.
Matumizi ya - o-o-te (wowote-yoyote)
Uuaji wowote unalaaniwa. Mauaji yoyote yanalaaniwa.
Matumizi ya –ngi ( mwingi- mengi)
Ubua mwingi umeteketea. Mabua mengi yameteketea.
Matumizi ya -ngine (mwingine-mengine)
Uamuzi mwingine haufai. Maamuzi mengine hayafai.
Matumizi ya -enye (wenye –yenye)
Ulezi wa mtoto uwe wenye mapenzi. Malezi ya watoto yawe yenye mapenzi.
Matumizi ya -enyewe (wenyewe-yenyewe)
Uongozi wenyewe unatisha. Maongozi yenyewe yanatisha.
Matumizi ya -ndi- (ndio-ndiyo)
Upishi ndio ulionipendeza. Mapishi ndiyo yaliyotupendeza.
Matumizi ya si- (sio-siyo)
Umbo huu sio kama ule. Maumbo haya siyo kama yale.
Matumizi ya na- (nao- nayo)
Ugonjwa ule nao ulimlemaza. Magonjwa yale nayo yaliwalemaza.
Kirejeshi amba- (ambao- ambayo)
Unyoya ambao unaota ni wa ndege. Manyoya ambayo yanaota ni ya ndege.
Kirejeshi o awali (o-yo)
Unyoya unaoota ni wa ndege. Manyoya yanayoota ni ya ndege.
Kirejeshi o tamati (o-yo)
Unyoya uotao ni wa ndege. Manyoya yaotayo ni ya ndege.

UKANUSHAJI KATIKA NYAKATI MBALIMBALI

Wakati uliopita (li) (hauku-hayaku)
Ulezi wa mtoto ulipendeza. Ulezi wa mtoto haukupendeza.
Malezi ya watoto yalipendeza. Malezi ya watoto hayakupendeza.
Wakati timilifu (me) (hauja-hayaja)
Ulezi wa mtoto umependeza. Ulezi wa mtoto haujapendeza.
Malezi ya watoto yamependeza. Malezi ya watoto hayajapendeza.
Wakati uliopo (na) (hau-haya)
Ulezi wa mtoto unapendeza. Ulezi wa mtoto haupendezi.
Malezi ya watoto yanapendeza. Malezi ya watoto hayapendezi.
Wakati ujao (ta) (hauta-hayata)
Ulezi wa mtoto utapendeza. Ulezi wa mtoto hautapendeza.
Malezi ya watoto yatapendeza. Malezi ya watoto hayatapendeza.

NGELI YA ....YA-YA
Viashiria / Vionyeshi

haya hayo yale
Maji haya ni baridi. Maji haya ni baridi.
Marashi hayo ni ghali. Marashi hayo ni ghali.
Mawaidha yale yatafaa. Mawaidha yale yatafaa.

Viambishingeli (ya-ya)
Mafuta yalimwagika. Mafuta yalimwagika.
Kiunganifu a (ya-ya)
Maji ya bahari ni mengi. Maji ya bahari ni mengi.
Matumizi ya ote (yote-yote)
Mazingira yote yatunzwe. Mazingira yote yatunzwe.
Matumizi ya - o-o-te (yoyote-yoyote)
Mali yoyote hunufaisha. Mali yoyote hunufaisha.
Matumizi ya–ngi ( mengi- mengi)
Maziwa mengi yamechemshwa. Maziwa mengi yamechemshwa.
Matumizi ya -ngine (mengine-mengine)
Maarifa mengine yatumiwe. Maarifa mengine yatumiwe.
Matumizi ya -enye (yenye –yenye)
Mawaidha yenye busara ni haya. Mawaidha yenye busara ni haya.
Matumizi ya -enyewe (yenyewe-yenyewe)
Marashi yenyewe yananukia. Marashi yenyewe yananukia.
Matumizi ya -ndi- (ndiyo-ndiyo)
Maendeleo ndiyo aliyoyatarajia. Maendeleo ndiyo waliyoyatarajia.
Matumizi ya si- (siyo-siyo)
Maisha yake siyo mema. Maisha yao siyo mema.
Matumizi ya na- (nayo- nayo)
Masika haya nayo yana mbu. Masika haya nayo yana mbu.
Kirejeshi amba- (ambayo- ambayo)
Maisha ambayo yanaudhi ni haya. Maisha ambayo yanaudhi ni haya.
Kirejeshi o awali (yo-yo)
Maisha yanayoudhi ni haya. Maisha yanayoudhi ni haya.
Kirejeshi o tamati (yo-yo)
Maisha yaudhiyo ni haya. Maisha yaudhiyo ni haya.

UKANUSHAJI KATIKA NYAKATI MBALIMBALI
Wakati uliopita (li) (hayaku-hayaku)
Maziwa yote yaliuzwa. Maziwa yote hayakuuzwa.
Wakati timilifu (me) (hayaja-hayaja)
Maziwa yote yameuzwa. Maziwa yote hayajauzwa.
Wakati uliopo (na) (haya-haya)
Maziwa yote yanauzwa. Maziwa yote hayauzwi.
Wakati ujao (ta) (hayata-hayata)
Maziwa yote yatauzwa. Maziwa yote hayatauzwa.

NGELI YA ....U-ZI
Viashiria / Vionyeshi
huu huo ule
hizi hizo zile
Uzi huu ni mdogo. Nyuzi hizi ni ndogo.
Wimbo huo ungeudhi. Nyimbo hizo zingeudhi.
Wakati ule ulikuwa mfupi. Nyakati zile zilikuwa fupi.

Viambishingeli (u-zi)
Ubavu unakuuma. Mbavu zinawauma.
Kiunganifu a (wa-za)
Ubawa huu ni wa ndege yupi? Mbawa hizi ni za ndege wapi?
Matumizi ya ote (wote-zote)
Uteo wote uliharibika. Teo zote ziliharibika.
Matumizi ya - o-o-te (wowote-zozote)
Wimbo wowote usiimbwe. Nyimbo zozote zisiimbwe.
Matumizi ya –ngi (mwingi-nyingi)
Wakati mwingi hupotezwa. Nyakati nyingi hupotezwa.
Matumizi ya -ngine (mwingine-nyingine)
Wembe mwingine utanunuliwa. Nyembe nyingine zitanunuliwa.
Matumizi ya -enye (wenye – zenye)
Wavu wenye samaki umekatika. Nyavu zenye samaki zimekatika.
Matumizi ya -enyewe (wenyewe-zenyewe)
Uwele wenyewe haujapona. Ndwele zenyewe hazijapona.
Matumizi ya -ndi- (ndio-ndizo)
Unywele ndio uliogeuka rangi. Nywele ndizo zilizogeuka rangi.
Matumizi ya si- (sio-sizo)
Wimbo huo sio wa zamani. Nyimbo hizo sizo za zamani.
Matumizi ya na- (nao-nazo)
Moyo wa mtu nao una siri. Nyoyo za watu nazo zina siri.
Kirejeshi amba- (ambao-ambazo)
Upi wembe ambao unakata? Zipi nyembe ambazo zinakata?
Kirejeshi o awali (o-zo)
Upi wembe unaokata? Zipi nyembe zinazokata?
Kirejeshi o tamati (o-zo)
Upi wembe ukatao? Zipi nyembe zikatazo?
UKANUSHAJI KATIKA NYAKATI MBALIMBALI
Wakati uliopita (li) (hauku-haziku)
Ufito ulikatwa. Ufito haukukatwa.
Fito zilikatwa. Fito hazikukatwa.
Wakati timilifu (me) (hauja-hazija)
Ufito umekatwa. Ufito haujakatwa.
Fito zimekatwa. Fito hazijakatwa.
Wakati uliopo (na) (hau-hazi)
Ufito unakatwa. Ufito haukatwi.
Fito zinakatwa. Fito hazikatwi.
Wakati ujao (ta) (hauta-hazita)
Ufito utakatwa. Ufito hautakatwa
Fito zitakatwa. Fito hazitakatwa.

NGELI YA ....U-U
Viashiria / Vionyeshi
huu huo ule
Wema huu ulimfaidi. Wema huu uliwafaidi.
Ujanja huo ulimponya. Ujanja huo uliwaponya.
Unga ule ulikuwa mweupe. Unga ule ulikuwa mweupe.

Viambishingeli (u-u)
Uwongo utajulikana. Uwongo utajulikana.
Kiunganifu a (wa-wa)
Ugali wa leo ni mtamu. Ugali wa leo ni mtamu.
Matumizi ya ote (wote-wote)
Uji wote umepozwa. Uji wote umepozwa.
Matumizi ya - o-o-te (wowote-wowote)
Udhalimu wowote utashindwa. Udhalimu wowote utashindwa.
Matumizi ya –ngi ( mwingi- mwingi)
Ameula ugali mwingi. Wameula ugali mwingi.
Matumizi ya -ngine (mwingine-mwingine)
Wino mwingine utanunuliwa. Wino mwingine utanunuliwa.
Matumizi ya -enye (wenye –wenye)
Uji wenye sukari ni mtamu. Uji wenye sukari ni mtamu.
Matumizi ya -enyewe (wenyewe-wenyewe)
Uwongo hujitenga wenyewe. Uwongo hujitenga wenyewe.
Matumizi ya -ndi- (ndio-ndio)
Moto ndio uchomao. Moto ndio uchomao.
Matumizi ya si- (sio-sio)
Usiku sio wa kuogofya. Usiku sio wa kuogofya.
Matumizi ya na- (nao- nao)
Ujana huu nao ni mfupi. Ujana huu nao ni mfupi.
Kirejeshi amba- (ambao- ambao)
Unga ambao unasagwa ni upi? Unga ambao unasagwa ni upi?
Kirejeshi o awali (o-o)
Unga unaosagwa ni upi? Unga unaosagwa ni upi?
Kirejeshi o tamati (o-o)
Unga usagwao ni upi? Unga usagwao ni upi?

UKANUSHAJI KATIKA NYAKATI MBALIMBALI
Wakati uliopita (li) (hauku-hauku)
Ukweli ulijulikana. Ukweli haukujulikana.
Wakati timilifu (me) (hauja-hauja)
Ukweli umejulikana. Ukweli haujajulikana.
Wakati uliopo (na) (hau-hau)
Ukweli unajulikana. Ukweli haujulikani.
Wakati ujao (ta) (hauta-hauta)
Ukweli utajulikana. Ukweli hautajulikana.

NGELI YA ....KU-KU
Viashiria / Vionyeshi
huku huko kule
Kuimba huku kumeniburudisha. Kuimba huku kumetuburudisha.
Kucheza huko kutaburudisha. Kucheza huko kutaburudisha.
Kuchora kule kunaibua hisia. Kuchora kule kunaibua hisia.

Viambishingeli (ku-ku)
Kulima kulikwisha jana. Kulima kulikwisha jana.
Kiunganifu a (kwa-kwa)
Kuchora kwa mtoto ni kuzuri. Kuchora kwa watoto ni kuzuri.
Matumizi ya ote (kote-kote)
Kuwinda kote kumekatazwa. Kuwinda kote kumekatazwa.
Matumizi ya - o-o-te (kokote-kokote)
Kucheka kokote hakufurahishi. Kucheka kokote hakufurahishi.
Matumizi ya –ngi ( kwingi- kwingi)
Kutembea kwingi kunaelimisha. Kutembea kwingi kunaelimisha.
Matumizi ya -ngine (kwingine-kwingine)
Kuongea kwingine kunaudhi. Kuongea kwingine kunaudhi.
Matumizi ya -enye (kwenye –kwenye)
Kusoma kwenye bidii ni kwema. Kusoma kwenye bidii ni kwema.
Matumizi ya -enyewe (kwenyewe-kwenyewe)
Kukwea kwenyewe kutachosha. Kukwea kwenyewe kutachosha.
Matumizi ya -ndi- (ndiko-ndiko)
Kuvua ndiko kutamfaidi mvuvi. Kuvua ndiko kutawafaidi wavuvi.
Matumizi ya si- (siko-siko)
Kutooga siko kuzuri. Kutooga siko kuzuri.
Matumizi ya na- (nako- nako)
Kuibiwa mjini nako kumezidi. Kuibiwa mijini nako kumezidi.
Kirejeshi amba- (ambako- ambako)
Kula ambako kunashibisha ni huku. Kula ambako kunashibisha ni huku.
Kirejeshi o awali (ko-ko)
Kula kunakoshibisha ni huku. Kula kunakoshibisha ni huku.
Kirejeshi o tamati (ko-ko)
Kula kushibishako ni huku. Kula kushibishako ni huku.

UKANUSHAJI KATIKA NYAKATI MBALIMBALI
Wakati uliopita (li) (hakuku-hakuku)
Kuchora kuliridhisha. Kuchora hakukuridhisha.
Wakati timilifu (me) (hakuja-hakuja)
Kuchora kumeridhisha. Kuchora hakujaridhisha.
Wakati uliopo (na) (haku-haku)
Kuchora kunaridhisha. Kuchora hakuridhishi.
Wakati ujao (ta) (hakuta-hakuta)
Kuchora kutaridhisha. Kuchora hakutaridhisha.

NGELI YA ....PA-KU-MU
Viashiria / Vionyeshi
hapa hapo pale
huku huko kule
humu humo mle
Hapa pamefagiliwa. Hapa pamefagiliwa.
Shuleni huko kumejengwa. Shuleni huko kumejengwa.
Chumbani mle mmesafishwa. Vyumbani mle mmesafishwa.

Viambishingeli (pa-ku-mu)
Pale alipo panafaa.. Pale walipo panafaa..
Mjini hakuendeki leo. Mijini hakuendeki leo.
Shuleni mmetulia. Shuleni mmetulia.
Kiunganifu a (pa-kwa-mwa)
Mahali pale ni pa kubarizia. Mahali pale ni pa kubarizia.
Kiotani kule ni kwa ndege. Viotani kule ni kwa ndege.
Mfukoni mwake mna sarafu. Mifukoni mwao mna sarafu.
Matumizi ya ote (pote-kote-mote)
Sijatembea pote mjini. Hatujatembea pote mijini.
Shambani kote kupaliliwe. Mashambani kote kupaliliwe.
Maji yamejaa bwawani mote. Maji yamejaa mabwawani mote.
Matumizi ya - o-o-te (popote-kokote-mokote)
Popote pasilimwe shambani. Popote pasilimwe mashambani.
Kokote kulimwe ili kupandwe michai. Kokote kulimwe ili kupandwe michai.
Mna giza momote chumbani. Mna giza momote vyumbani.
Matumizi ya –ngi (pengi- kwingi- mwingi)
Sokoni pengi ni pachafu. Masokoni pengi ni pachafu.
Jangwani kwingi kuna changarawe. Majangwani kwingi kuna changarawe.
Majini mwingi mna viini. Majini mwingi mna viini.
Matumizi ya -ngine (pengine-kwingine-mwingine)
Mahali pengine pana baridi kali. Mahali pengine pana baridi kali.
Kule kwingine kuna mgeni. Kule kwingine kuna wageni.
Dukani mwingine hamna mizani. Madukani mwingine hamna mizani.
Matumizi ya -enye (penye-kwenye –mwenye)
Msituni penye chui panaogofya. Misituni penye chui panaogofya.
Mtoni kwenye maji kunafuliwa nguo. Mtoni kwenye maji kunafuliwa nguo.
Shimoni mwenye nyoka ni hatari. Mashimoni mwenye nyoka ni hatari.
Matumizi ya -enyewe (penyewe-kwenyewe-mwenyewe)
Mahali penyewe hapakutajwa. Mahali penyewe hapakutajwa.
Kwake kwenyewe ku mbali sana. Kwao kwenyewe ku mbali sana.
Pangoni mwenyewe mnaye nyoka. Mapangoni mwenyewe mnao nyoka.
Matumizi ya -ndi- (ndipo-ndiko-ndimo)
Hapa ndipo alipopalima. Hapa ndipo walipopalima.
Huku ndiko kunako mali. Huku ndiko kunako mali.
Nyumbani ndimo mlimo jamaa zangu. Nyumbani ndimo mlimo jamaa zetu.
Matumizi ya si- (sipo-siko-simo)
Shuleni pale sipo alipopasomea. Shuleni pale sipo walipopasomea.
Sokoni siko kuuzwako mihadarati. Masokoni siko kuuzwako mihadarati.
Shambani mle simo mlimolimwa. Mashambani mle simo mlimolimwa.
Matumizi ya na- (napo-nako- namo)
Kanisani napo panaabudiwa Mungu. Makanisani napo panaabudiwa Mungu.
Kule kwake nako kuna sherehe. Kule kwao nako kuna sherehe.
Ziwani namo mna samaki. Maziwani namo mna samaki.
Kirejeshi amba- (ambapo-ambako- ambamo)
Shuleni ambapo panasomewa ni hapa. Shuleni ambapo panasomewa ni hapa.
Shuleni ambako kunasomewa ni huku. Shuleni ambako kunasomewa ni huku.
Shuleni ambamo mnasomewa ni humu.-Shuleni ambamo mnasomewa ni humu.
Kirejeshi o awali (po-ko-mo)
Shuleni panaposomewa ni hapa. Shuleni panaposomewa ni hapa.
Shuleni kunakosomewa ni huku. Shuleni kunakosomewa ni huku.
Shuleni mnamosomewa ni humu. Shuleni mnamosomewa ni humu.
Kirejeshi o tamati (po-ko-mo)
Shuleni pasomewapo ni hapa. Shuleni pasomewapo ni hapa.
Shuleni kusomewako ni huku. Shuleni kusomewako ni huku.
Shuleni msomewamo ni humu. Shuleni msomewamo ni humu.

UKANUSHAJI KATIKA NYAKATI MBALIMBALI

Wakati uliopita (li) (hapaku-hakuku-hamku)
Mbugani pale palipendeza. Mbugani pale hapakupendeza.
Mbugani kule kulipendeza. Mbugani kule hakukupendeza.
Mbugani mle mlipendeza. Mbugani mle hamkupendeza.
Wakati timilifu (me) (hapaja-hakuja-hamja)
Mbugani pale pamependeza. Mbugani pale hapajapendeza.
Mbugani kule kumependeza. Mbugani kule hakujapendeza.
Mbugani mle mmependeza. Mbugani mle hamjapendeza.
Wakati uliopo (na) (hapa-haku-ham)
Mbugani pale panapendeza. Mbugani pale hapapendezi.
Mbugani kule kunapendeza. Mbugani kule hakupendezi.
Mbugani mle mnapendeza. Mbugani mle hampendezi.
Wakati ujao (ta) (hapata-hakuta-hamta)
Mbugani pale patapendeza. Mbugani pale hapatapendeza
Mbugani kule kutapendeza. Mbugani kule hakutapendeza.
Mbugani mle mtapendeza. Mbugani mle hamtapendeza.

NGELI YA ....I-I
Viashiria / Vionyeshi
hii hiyo ile
Miwani hii ni yake. Miwani hii ni yao.
Mihadarati hiyo ni hatari. Mihadarati hiyo ni hatari.
Mizani ile haipimi vizuri. Mizani ile haipimi vizuri

Viambishingeli (i-i)
Miwani yangu imeletwa. Miwani yetu imeletwa.
Kiunganifu a (ya-ya)
Mizani ya kupimia imenunuliwa. Mizani ya kupimia imenunuliwa.
Matumizi ya ote (yote-yote)
Mihirabu yote imesafishwa. Mihirabu yote imesafishwa.
Matumizi ya - o-o-te (yoyote-yoyote)
Mirimo yoyote yenye faida ifanywe. Mirimo yoyote yenye faida ifanywe.
Matumizi ya -ngi (mingi)
Miraa mingi hukuzwa Meru.
Matumizi ya -ngine (mingine-mingine)
Mirathi mingine imepewa mwana. Mirathi mingine imepewa wana.
Matumizi ya -enye (yenye -yenye)
Elimu ni mirathi yenye faida. Elimu ni mirathi yenye faida..
Matumizi ya -enyewe (yenyewe-yenyewe)
Miwani yenyewe humsaidia. Miwani yenyewe huwasaidia.
Matumizi ya -ndi- (ndiyo-ndiyo)
Midadi hii ndiyo iliyoandikiwa ukurasa. Midadi hii ndiyo iliyoandikiwa kurasa.
Matumizi ya si- (siyo-siyo)
Miwani siyo iwekwayo ovyo. Miwani siyo iwekwayo ovyo.
Matumizi ya na- (nayo- nayo)
Miadi ile nayo imetimizwa. Miadi ile nayo imetimizwa.
Kirejeshi amba- (ambayo- ambayo)
Mirimo ambayo inafanywa ni migumu. Mirimo ambayo inafanywa ni migumu.
Kirejeshi o awali (yo-yo)
Mirimo inayofanywa ni migumu. Mirimo inayofanywa ni migumu.
Kirejeshi o tamati (yo-yo)
Mirimo ifanywayo ni migumu. Mirimo ifanywayo ni migumu.

UKANUSHAJI KATIKA NYAKATI MBALIMBALI
Wakati uliopita (li) (haiku-haiku)
Miraa ilipandwa. Miraa haikupandwa.
Wakati timilifu (me) (haija-haija)
Miraa imepandwa. Miraa haijapandwa.
Wakati uliopo (na) (hai-hai)
Miraa inapandwa. Miraa haipandwi.
Wakati ujao (ta) (haita-haita)
Miraa itapandwa. Miraa haitapandwa.

Sunday, September 13, 2009

Kukanusha

UKANUSHAJI

• Wakati uliopita (li)

Mimi nilikisoma kitabu hiki. Mimi sikukisoma kitabu hiki.
Sisi tulivisoma vitabu hivi. Sisi hatukuvisoma vitabu hivi.

Wewe ulienda mjini. Wewe hukuenda mjini.
Nyinyi mlienda mijini. Nyinyi hamkuenda mijini.

Yeye aliipenda anasa. Yeye hakuipenda anasa.
Wao walizipenda anasa. Wao hawakuzipenda anasa.

• Wakati timilifu (me)

Mimi nimekisoma kitabu hiki. Mimi sijakisoma kitabu hiki
Sisi tumevisoma vitabu hivi. Sisi hatujavisoma vitabu hivi.

Wewe umeenda mjini. Wewe hujaenda mjini.
Nyinyi mmeenda mjini. Nyinyi hamjaenda mijini.

Yeye ameipenda anasa. Yeye hajaipenda anasa.
Wao wamezipenda anasa. Wao hawajazipenda anasa.

• Wakati uliopo (na)

Mimi ninakisoma kitabu hiki. Mimi sikisomi kitabu hiki.
Sisi tunavisoma vitabu hivi. Sisi hatuvisomi vitabu hivi.

Wewe unaenda mjini. Wewe huendi mjini.
Nyinyi mnaenda mjini. Nyinyi hamwendi mijini.

Yeye anaipenda anasa. Yeye haipendi anasa.
Wao wanazipenda anasa. Wao hawazipendi anasa.

• Wakati ujao (ta)

Mimi ni nitakisoma kitabu hiki. Mimi sitakisoma kitabu hiki.
Sisi tu tutavisoma vitabu hivi. Sisi hatutavisoma vitabu hivi.

Wewe utaenda mjini. Wewe hutaenda mjini.
Nyinyi mtaenda mijini. Nyinyi hamtaenda mijini.

Yeye ataipenda anasa. Yeye hataipenda anasa.
Wao watazipenda anasa. Wao hawatazipenda anasa.